.

.
.

.

.
.

.

.

Saturday, June 9, 2018

CHUO CHA UALIMU NYAMAHANGA

Chuo cha Ualimu Nyamahanga Ni chuo kilichopo mkoani Kagera wilaya ya Biharamulo kata ya Nyamahanga kipo umbali wa kilomita tisa kutoka Biharamulo Mjini kwenye barabara ya kuelekea Lusahunga na kipo chini ya Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania.

Chuo kilisajiliwa mwaka 2006 kikiwa na lengo la kutoa elimu na maadili mema   na hadi sasa Chuo kimehitimisha jumla ya walimu elfu moja mia tano thelathini na tatu wa daraja A na wamefanikiwa kupata ajira za serikali.

Chuo hiki kina mandhari mazuri ya kujifunzia yatakayomuwezesha mwanachuo kufanya vizuri katika masomo yake.Chuo kimezungukwa na milima yenye uoto wa asili ambayo husababisha mazingira ya chuo kuwa na hewa safi muda wote.

Kuna wakufunzi waliobobea katika fani ya ufundishaji,kuna madarasa na mabweni ya kutosha wanachuo wote,kuna umeme wa uhakika na inapotokea umeme wa Tanesco kukatika chuo kina umeme wa generator na umeme wa nishati ya jua.

Maji yapo ya kukidhi mahitaji ya wanachuo,kuna kituo cha afya kuwahudumia wanachuo na wananchi wanaozunguka maeneo yote ya chuo,kuna viwanja vya michezo kuwawezesha wanachuo kujenga mwili kiafya  na mengine mengi.


Baadhi ya wanachuo wakicheza mpira wa wavu.

Baada ya muda wa masomo wanachuo hupumzisha akili kwenye baadhi ya michezo kama inavyoonekana hapo juu.

Baadhi ya wanachuo wa mwaka wa pili wakiwa mbele ya jengo la utawala.

Wanachuo wakiwa wamesimama mbele ya darasa.

Saturday, June 2, 2018

NAFASI ZA KOZI YA UALIMU

Mkuu wa chuo cha ualimu Nyamahanga anatangaza nafasi ya kozi ya miaka miwili ya ualimu daraja "A" kwa mwaka wa masomo 2018/2019.

KWANINI UJIUNGE NA CHUO CHA UALIMU NYAMAHANGA?

  • Chuo kina miundo mbinu bora,madarasa yenye kiwango,Mabweni mazuri,Maktaba ya kompyuta.
  • Chuo kina Maktaba yenye vitabu vya kutosha, mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia na wakufunzi bora waliobobea katika ufundishaji.
  • Chuo kina ufaulu mzuri sana tangu kilipoanza hadi sasa.


 SIFA ZA MWOMBAJI:

  • Awe amehitimu kidato cha nne na mwenye ufaulu usiopungua Division III, Point 25.
KWA MAWASILIANO ZAIDI,KUPATA NA KUTUMA FOMU YA KUJIUNGA NA CHUO:


Mkuu wa Chuo,
Chuo cha Ualimu Nyamahanga,
S.L.P 25,
Biharamulo,
Kagera.

Email:nyamahangatc@gmail.com

Simu : 0688381381/ 0756281824 / 0767894537/ 0759329597
.

                                      Karibu sana Chuo cha Ualimu Nyamahanga
                                               "ELIMU NA MAADILI MEMA"