.

.
.

.

.
.

.

.

Saturday, June 9, 2018

CHUO CHA UALIMU NYAMAHANGA

Chuo cha Ualimu Nyamahanga Ni chuo kilichopo mkoani Kagera wilaya ya Biharamulo kata ya Nyamahanga kipo umbali wa kilomita tisa kutoka Biharamulo Mjini kwenye barabara ya kuelekea Lusahunga na kipo chini ya Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania.

Chuo kilisajiliwa mwaka 2006 kikiwa na lengo la kutoa elimu na maadili mema   na hadi sasa Chuo kimehitimisha jumla ya walimu elfu moja mia tano thelathini na tatu wa daraja A na wamefanikiwa kupata ajira za serikali.

Chuo hiki kina mandhari mazuri ya kujifunzia yatakayomuwezesha mwanachuo kufanya vizuri katika masomo yake.Chuo kimezungukwa na milima yenye uoto wa asili ambayo husababisha mazingira ya chuo kuwa na hewa safi muda wote.

Kuna wakufunzi waliobobea katika fani ya ufundishaji,kuna madarasa na mabweni ya kutosha wanachuo wote,kuna umeme wa uhakika na inapotokea umeme wa Tanesco kukatika chuo kina umeme wa generator na umeme wa nishati ya jua.

Maji yapo ya kukidhi mahitaji ya wanachuo,kuna kituo cha afya kuwahudumia wanachuo na wananchi wanaozunguka maeneo yote ya chuo,kuna viwanja vya michezo kuwawezesha wanachuo kujenga mwili kiafya  na mengine mengi.


Baadhi ya wanachuo wakicheza mpira wa wavu.

Baada ya muda wa masomo wanachuo hupumzisha akili kwenye baadhi ya michezo kama inavyoonekana hapo juu.

Baadhi ya wanachuo wa mwaka wa pili wakiwa mbele ya jengo la utawala.

Wanachuo wakiwa wamesimama mbele ya darasa.

1 comment:

  1. Nimefurahi sana kukijua chuo hiki, binafsi no muda sasa nimekuwa nakisikia tu takribani miaka 7 juu ya maadili ya chuo hiki, powerful institution. I like it.

    ReplyDelete